Deep and overstood, Swahili

MAMA ALIMPENDA (2010) …..to be continued


Harusi ilishafanyika

Wageni makwao wakaregea

Mapochopocho yalishatiririka

Na vitu za fahari nyumbani zikabombea

Usiku wa manane ulishafika

Babake na mamaye kitandani wakatokomea

Jumaa tatu mama hangestahimili kutapika

Maisha ya mwanaye tayari yashaanzia

Alikuwa msichana na hakuna makosa yaliyofanyika

Ingawa babake alimkana na kichapo mamake kumwagizia

Kwa yote haya, mama alimpenda

Tumboni mwa mamaye alielea na akatoka kama ameundwa

Miaka kadhaa na yule msichana keshageuka kuwa kidosho

Baba aliyemkana kamuona tayari kugeuka awe fedha

Darasa la nane keshafaulu, zawadi ashalifunga kwa leso

Gwaride la fisi wazee nje ya nyumba tayari kumposa

Kilio cha huyu kipenzi wa macho chawasilisha yake mateso

Kakake washaendelea shule ya upili, maombi yake yapuuzwa

Ila mamaye mtoto, hakuvunjika moyo

Kabembeleza mumewe abadili nia

Kidosho keshapata bahati, kaendelea masomo

Njia nyembamba maishani, mama alimpenda

Kidato cha kwanza, pili, tatu, cha nne kwishamalizia

Chuo kikuu kaingia, kuepuka madhara ya maisha

Wakufunzi wamsumbua, alama wamkazia

Mrembo kajikaza, vikwazo kaziruka

Miaka kadhaa kapita, kazini keshaingia……………………………………………

Deep and overstood, Hip hop, Kenya, Politricks, Swahili

UPAKATAJI WA MANENO


Ninapowasili kivuli changu ni Kiswahili.

Makofi yanayopigwa siyo yanayostahili.

Kuandika sio mashindano kwa hivyo nayastahimili.

Nyota ya majivuno haing’ai kwa changu kiwiliwili.

Nikifika, mbiu yangu yafanya mwaitika.

Binadamu wa kila kabila hata rika.

Nawaangalia kwa macho ya asiyetishika.

Maneno kwa akili naendelea kuyapika.

Kila siku niamkapo nikiwaza.

Fikira zanizunguka hadi ninapojilaza.

Mimi sio msanii kama Gaza.

Ni sauti ya moyo wangu ninayoipaza.

Ninaposhika yangu kalamu.

Sitaraji kuayaandika yaliyo matamu.

Lakini miye hushikwa na hamu.

Ndiposa naandika kama asiye na fahamu.

Ukitaka unaweza nidharau.

Lakini tupo wengi kwa hili dau.

Kwa mfano kabla sijasahau.

Lazima utakumbuka fulani wa ukoo wetu Mau Mau.

Haya maneno yananichesha

Sina habari na sijali kama nje kwanyesha.

Kupingana kwako nami hakutanichosha.

Kwani naamini shairi langu ni mambo tosha.

Kabla sijalitia kikomo.

Wacheni tuwakumbuke waliotuacha kwa kufunga yetu midomo.

Maisha mafupi ya aliyekuwa wangu somo.

Agosti miaka kumi na mitano iliyopita na wengine waliomo.

Kalamu yangu haitaisha wino labda kitabu kijae.

Najua kila mmoja wenu yuajua maana yake.

Nitazikunja zangu vidole na kuwafanya mshangae.

Lakini kwa sasa, wacheni twendelee baadaye.

Swahili

Kusakamwa ama kutokanywa?


Ukinibusu sitakufikiria tena
Ukinidharau kwako sitanena
Nisipomaliza kazi utafanya?
Hii kalamu nimeshikilia sijasanya.
Nikikimbia najikwaa
Nikitembea nachelewa
Nifikapo kwako napigwa na butwaa
Maneno yangu wakataa kuyaelewa
Uwe mwalimu ama mpenzi wangu
Kilicho muhimu ni kwamba maisha ni yangu

Maisha ni yako?
Nani kakudanganya?
Mwili si wako hata matako.
Salala matakwa nimejikanganya.
Ukiwa wewe kisiwa basi maji ni nani?
Bila ziwa wewe ni mlima pweke
Sitaki kukusukuma maishani
Lakini mawaidha yangu uyaweke.
Nikikuzaba kofi usilie.
Kabla uchome nyumba yangu,si ufikirie?