Harusi ilishafanyika
Wageni makwao wakaregea
Mapochopocho yalishatiririka
Na vitu za fahari nyumbani zikabombea
Usiku wa manane ulishafika
Babake na mamaye kitandani wakatokomea
Jumaa tatu mama hangestahimili kutapika
Maisha ya mwanaye tayari yashaanzia
Alikuwa msichana na hakuna makosa yaliyofanyika
Ingawa babake alimkana na kichapo mamake kumwagizia
Kwa yote haya, mama alimpenda
Tumboni mwa mamaye alielea na akatoka kama ameundwa
Miaka kadhaa na yule msichana keshageuka kuwa kidosho
Baba aliyemkana kamuona tayari kugeuka awe fedha
Darasa la nane keshafaulu, zawadi ashalifunga kwa leso
Gwaride la fisi wazee nje ya nyumba tayari kumposa
Kilio cha huyu kipenzi wa macho chawasilisha yake mateso
Kakake washaendelea shule ya upili, maombi yake yapuuzwa
Ila mamaye mtoto, hakuvunjika moyo
Kabembeleza mumewe abadili nia
Kidosho keshapata bahati, kaendelea masomo
Njia nyembamba maishani, mama alimpenda
Kidato cha kwanza, pili, tatu, cha nne kwishamalizia
Chuo kikuu kaingia, kuepuka madhara ya maisha
Wakufunzi wamsumbua, alama wamkazia
Mrembo kajikaza, vikwazo kaziruka
Miaka kadhaa kapita, kazini keshaingia……………………………………………