Ninapowasili kivuli changu ni Kiswahili.
Makofi yanayopigwa siyo yanayostahili.
Kuandika sio mashindano kwa hivyo nayastahimili.
Nyota ya majivuno haing’ai kwa changu kiwiliwili.
Nikifika, mbiu yangu yafanya mwaitika.
Binadamu wa kila kabila hata rika.
Nawaangalia kwa macho ya asiyetishika.
Maneno kwa akili naendelea kuyapika.
Kila siku niamkapo nikiwaza.
Fikira zanizunguka hadi ninapojilaza.
Mimi sio msanii kama Gaza.
Ni sauti ya moyo wangu ninayoipaza.
Ninaposhika yangu kalamu.
Sitaraji kuayaandika yaliyo matamu.
Lakini miye hushikwa na hamu.
Ndiposa naandika kama asiye na fahamu.
Ukitaka unaweza nidharau.
Lakini tupo wengi kwa hili dau.
Kwa mfano kabla sijasahau.
Lazima utakumbuka fulani wa ukoo wetu Mau Mau.
Haya maneno yananichesha
Sina habari na sijali kama nje kwanyesha.
Kupingana kwako nami hakutanichosha.
Kwani naamini shairi langu ni mambo tosha.
Kabla sijalitia kikomo.
Wacheni tuwakumbuke waliotuacha kwa kufunga yetu midomo.
Maisha mafupi ya aliyekuwa wangu somo.
Agosti miaka kumi na mitano iliyopita na wengine waliomo.
Kalamu yangu haitaisha wino labda kitabu kijae.
Najua kila mmoja wenu yuajua maana yake.
Nitazikunja zangu vidole na kuwafanya mshangae.
Lakini kwa sasa, wacheni twendelee baadaye.
Reblogged this on hypnoticfruition.